NENO LENYE AMANI NDANI YANGU Read Count : 83

Category : Articles

Sub Category : Self Help
Sauti zao si njema, sura zao si mbaya, 
Ila wenye kukinaisha na kuhuzunisha, 
Matendo yao hayana uungwana, 
Hujibebebesha mizigo ya hakuna, 
Huku hofu ya vilalama ikitetemesha anga,
Si usiku ama mchana, kiangazi ama masika,
Dunia imevurugwa na kondeni tunaswagwa,
Neno lenye nguvu ni lipi? 
Ili tuwakumbushe kuwa ni kheri kula mlo mmoja katika amani kuliko kuishi kwa tabu na Mali zetu mkononi?
Ni ipi njaa mbaya zaidi katika haya? 
Kukosa chakula ama kupakumbuka nyumbani kwenu harafu uwezo wa kufika huna? 
Iteremsheni amani ili dunia na waamkao wauone ukuu na unyenyekevu was watu wangu.


Comments

  • good

    Jun 30, 2020

Log Out?

Are you sure you want to log out?